Sunday, 11 September 2016

TETEMEKO LAFANYA UHARIBIFU KANDA YA ZIWA

Picha: Tetemeko la ukubwa wa 5.7 lasababisha vifo Mwanza na Kagera

Tetemeko lenye ukubwa (magnitude) wa 5.7 limetokea mchana, Jumamosi hii katika mikoa ya Mwanza, Kagera na sehemu za Shinyangabukoba10
Baadhi ya nyumba zimebomoka na kujeruhi watu. Hadi sasa zaidi ya watu 10 wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwabukoba11
“Nimelishuhudia Misungwi hatari nyumba inatikisika unaona kabisa .. Tuzidisheni ibada jamani,” ameandika mwananchi mmoja kwenye Facebook.cr_3zaswiaaj3xt
Mwanza tumehaha, tetemeko limenikuta nipo ndani nakula, tukawa tumetoka nje ili kupisha tusije kudondokewa na nyumba, ile tetemeko limeisha tukarudi ndani, ile tunarudi ndani tetemeko likaanza tena. Lakini tunamshukuru Mungu kwetu limepita salama, pole kwa waliopatwa na maafa,” ameandika mwingine.
“Limedumu kwa muda wa zaidi ya dakika tatu huku Simiyu mwishowe lilimalizia kwa kishindo watu wametaharuki sana,” ameandika mwananchi mwingine.
Tetemeko hilo limesababisha taharuki kubwa kwa wakazi wa maeneo ya Mwanza na Kagera. Hizi ni picha zaidi za nyumba zilizoathirika.
“Daaaaa!!ilikuwa ni shiida yaan tetemeko hili cjawahi kushuhudia limekaa muda mrefu kwel yaan nilikuwa nimelala nyumba ilivyotingishika had kitanda kikawa kinahama toka sehem moja kwenda nyingine Mungu baba nakuomba hii hali isirudie tena baba,” ameandika mkazi wa Mwanza, Boniface Shayo.
whatsapp-image-2016-09-10-at-15-59-12

cr_5wmuxeaapree
cr_30pkxeaaqqf7
image-1
image-2
image

No comments:

Post a Comment